Wanafuzi wa darasa la tano wajifunza somo la sayansi kwa vitendo
Wanafunzi wa Darasa la Tano walifanya somo la Sayansi kwa njia ya vitendo wakijifunza kuhusu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kupitia uchunguzi wa kuku. Shughuli hii iliwapa fursa ya kuona kwa uhalisia sehemu mbalimbali za mfumo wa mmeng’enyo na kuelewa kazi zake katika mwili wa kiumbe hai.
Kupitia somo hilo, wanafunzi waliweza:
Kutambua sehemu kuu za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Kuelewa mchakato wa mmeng’enyo kwa njia ya vitendo
Kukuza ujuzi wa uchunguzi na kujifunza kwa uzoefu halisi
Shule inaendelea kutumia mbinu shirikishi na za vitendo ili kuimarisha uelewa wa wanafunzi katika Sayansi na kuwajengea msingi imara wa maarifa.
Ofisi ya Taaluma itaendelea kusimamia utekelezaji wa masomo ya vitendo ili kukuza ubunifu, udadisi, na ufaulu wa wanafunzi.